Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM waadhimisha Siku ya Kukomesha Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki

UM waadhimisha Siku ya Kukomesha Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki

Mapema wiki hii UM uliandaa taadhima mbalimbali kwenye Makao Makuu mjini New York, kuheshimu ile siku ambayo miaka 200 nyuma kulipitishwa sheria nchini Uingereza kukomesha biashara ya kuchuuza wanadamu, kama bidhaa, kati ya mataifa yaliopo ng’ambo ya Bahari ya Atlantiki.~~

Kwenye makala ya kipindi tumekupatieni dokezo ya risala ya Naibu KM Asha-Rose Migiro juu ya taadhima za Siku ya Kukomesha Biashara ya Utumwa mnamo miaka 200 iliopita, risala ambayo vile vile iligusia tatizo la utumwa mambo leo. Kadhalika tumejumuisha mahojiano na Profesa Ali Mazrui wa Chuo Kikuu cha New York-Binghamton, ambapo anachambua na kufafanua athari za biashara ya utumwa kwa vizazi vya Waafrika walioibiwa makwao na kupelekwa Marekani na Visiwa vya Karibian.

Kwa maelezo kamili sikiliza idhaa ya mtandao.