Profesa Ali Mazrui wa Chuo Kikuu cha New York-Binghamton juu ya msiba wa biashara ya utumwa

30 Machi 2007

Mnamo tarehe 25 Machi 1807 Bunge la Uingereza lilipitisha sheria ya kupiga marufuku jahazi zote za Kiingereza kusafirisha, kile walichokiita, bidhaa ya wanadamu, yaani ile biashara ya kuvusha watu waliotekwa nyara makwao katika Bara la Afrika, na ambao walisafirishwa mataifa ya ng\'ambo ya Bahari ya Atlantiki kufanya kazi ya utumwa, hususan katika Amerika na Visiwa vya Karibian.

Kwenye mahojiano aliyokuwa nayo na Idhaa ya Redio ya UM, Profesa Mazrui alisailia historia fupi ya miaka 200 tangu biashara ya utumwa kukomeshwa, na vile vile alifafanua athari za msiba wa utumwa kwa vizazi vilivyofuatia.

Kwa mahojiano kamili sikiliza idhaa ya mtandao.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter