Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi za kimataifa za kuboresha maisha kwa wakazi wa mitaa ya mabanda Afrika Mashariki (Sehemu ya Kwanza)

Juhudi za kimataifa za kuboresha maisha kwa wakazi wa mitaa ya mabanda Afrika Mashariki (Sehemu ya Kwanza)

Hivi karibuni, aliyekuwa mwandishi habari wa Idhaa ya Redio ya UM, Michele Montas alizuru Kenya kuangalia namna mashirika wenzi na UM yanavyoendeleza huduma za kupunguza umasikini, hasa miongoni mwa ule umma wenye kuishi kwenye mazingira ya hali duni.

Mwanahabari huyo Redio ya UM alifanya mahojiano na wakazi wa Mathare juu ya matatizo yao, namna wanavyokabiliana nayo, na kusailia huduma za maendeleo za mashirika yasio ya kiserekali, mathalan GROOTS-Mathare, shirika ambalo huwapatia wakazi wa eneo hilo la mji mafunzo ya kazi za ushoni na pia huduma ya uuguzaji wa majumbani.

Kwa mahojiano kamili sikiliza idhaa ya mtandao.