16 Februari 2007
Alkhamisi Mshauri wa KM juu ya Masuala ya Kisiasa, Tuliameni Kalomoh aliwasilisha risala maalumu ya KM Ban Ki-moon kwenye Mkutano Mkuu wa siku tano juu ya hatua za kuimarisha uhusiano kati ya Afrika na Ufaransa uliofanyika kwenye mji wa Cannes, Ufaransa. Viongozi wa kutoka mataifa kadha ya Afrika pamoja na Ufaransa walihudhuria mkusanyiko huo.