12 Januari 2007
Mjumbe Maalumu wa UM kwa Darfur, Jan Eliasson wa Usweden anatazamiwa kukamilisha ziara yake rasmi katika Sudan wiki hii. Alifanikiwa kuonana kwa mazungumzo na viongozi kadha wa kadha wa Serekali ya Sudan na pia wale wanaowakilisha makundi ya waasi waliotia sahihi Maafikiano ya Abuja na wale wasioridhia itifaki hiyo.