Skip to main content

Kumbukumbu za mkutano wa awali wa KM mpya na vyombo vya habari

Kumbukumbu za mkutano wa awali wa KM mpya na vyombo vya habari

KM Ban Ki-moon alifanyisha mkutano rasmi wa kwanza na wawakilishi wa vyombo vya habari vya kimataifa waliopo Makao Makuu ya UM mjini New York mnamo Alkhamisi ya tarehe 11 Januari 2007. KM Ban aliwafafanulia ratiba ya masuala aliyokabiliana nayo siku 10 baada ya kuchukua madaraka ya kuongoza taasisi hii muhimu ya kimataifa.

KM aliahidi kuyapa umuhimu unaostahiki yale masuala yanayofungamana na maendeleo katika bara la Afrika, katika kufufua huduma za uchumi, kusawazisha utulivu wa jamii na vile vile kuimarisha shughuli za usalama na amani.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.