Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuo Kikuu cha Pretoria kutunukiwa zawadi ya UNESCO

Chuo Kikuu cha Pretoria kutunukiwa zawadi ya UNESCO

Kitivo cha Haki za Kiutu cha Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini kinachosimamia mafunzo yanayohusu taratibu za kuimarisha haki za kimsingi kimetunukiwa zawadi ya dola 10,000 na Shirika la Umoja wa Mataifa juu ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO).

Kitivo cha Haki za Kiutu kilisaidia kupitisha mswada wa haki za raia na katika maandalizi ya mpango wa kujenga kanuni za katiba.