Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya kimataifa imeahidi kuimarisha Mpango wa Kimberley dhidi ya 'almasi za damu'

Jamii ya kimataifa imeahidi kuimarisha Mpango wa Kimberley dhidi ya 'almasi za damu'

Hivi majuzi, Baraza Kuu la UM lilipitisha azimio muhimu liliosisitiza ya kwamba jamii ya kimataifa inawajibika kuendelea kuunga mkono juhudi za pamoja za kuboresha udhibiti wa biashara haramu ya almasi duniani.

Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika UM, Balozi Augustine Mahiga anatufafanulia, kwenye mazungumzo na Idhaa ya Redio ya Umoja wa Mataifa, nini hasa Mpango wa Kimberley humaanisha.

Sikiliza mahojiano katika mtandao.