Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hapa na pale.

Hapa na pale.

KM mpya wa UM, Ban Ki-moon anatazamiwa kuanza kazi rasmi mnamo Ijumanne, tarehe 02 Januari 2007. ~

• Muhammad ElBaradei, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la UM juu ya Matumizi ya Amani ya Nishati ya Nyuklia (IAEA) amenasihi ya kuwa mvutano kuhusu haki ya Iran kusafisha yuraniamu halisi kwenye viwanda vyake vya nishati unaweza kutatuliwa kwa suluhu ya amani, ya muda mrefu, na ya kuridhisha, pindi jamii ya kimataifa itajihusisha, kwa moyo safi, kwenye majadiliano ya jumla, ya ushirikiano wa kuheshimiana.

•Ofisi ya UM juu ya Misaada ya Kiutu (OCHA) imeripoti kwamba ule Mfuko wa Dharura ujulikanao kama Mfuko wa CERF, umefanikiwa kuhudumia mipango ya dharura 328 katika nchi 31 kote duniani, miezi tisa baada ya mfuko huo kuanzishwa rasmi na jumuiya ya kimataifa.