UNHCR imeanzisha ugawaji mkuu wa nguo kwa wahamiaji wa DRC kabla ya majira ya mvua kuwasili

10 Novemba 2006

Shirika la UM juu ya huduma za Wahamiaji (UNHCR) karibuni limeanzisha huduma za ugawaji wa nguo kwa wakimbizi 50,000 ziada muhitaji waliopo kwenye kambi za Gety na Kagaba, katika Jimbo la Ituri.

Kadhalika, hivi karibuni UNHCR ililazimika kusitisha huduma za kuwarejesha makwao, kwa mashua, maelfu ya wahamiaji wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC)waliopo Tanzania kwa sababu ya kunyesha mvua kali katika jimbo la Kivu ya Kusini zilizosababisha miporomoko ya mawe na miamba, baadhi yao yakiwa na ukubwa wa malori, ambayo ilifunga zile njia panda zinazotumiwa na misafara ya UNHCR kuwahamishia umma huo kati ya Bandari ya Baraka na Uvira. UNHCR imeripoti iko tayari kuanzisha tena misafara hiyo haraka iwezekanavyo hali ya hewa ikitengenea.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter