Ripoti ya KM juu ya hali katika Sahara ya Magharibi

20 Oktoba 2006

Ripoti ya KM, iliyowasilishwa wiki hii kuhusu hali katika Sahara ya Magharibi imependekeza Baraza la Usalama kutoa mwito kwa Morocco na Chama cha Ukombozi wa Sahara ya Magharibi, Frente Polisario, wa kuwahimiza kushirki kwenye majadiliano yasio na shuruti, ya kutafuta suluhu ya kuridhisha na ya kudumu, itakayowawezesha wazalendo wa Sahara ya Magharibi hatimaye kutekelezewa haki ya kujiamulia wenyewe utawala halali.

Kadhalika, KM alitilia mkazo kwenye ripoti yake umuhimu wa mchango wa Shirika la UM linalosimamia Usimamishaji wa Mapigano katika Sahara ya Magharibi (MINURSO). Kwa hivyo KM alipendekeza muda wa kazi za MINURSO za kuimarisha utulivu wa eneo uongezwe kwa miezi sita ziada, hadi mwisho wa Aprili 2007.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud