Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 126 wakhofiwa kufa kwenye Ghuba ya Aden

Watu 126 wakhofiwa kufa kwenye Ghuba ya Aden

Shirika la UM juu ya Huduma za Wahamiaji (UNHCR)limeripoti kwamba katika wiki za karibuni watu 126 kutoka Afrika Mashariki walifariki au kupotea walipokuwa wanajaribu kuvuka Ghuba ya Aden baada ya kutupwa majini kutoka meli na mashua za wafanya magendo.

Kwa mujibu wa UNHCR wahamiaji hawa walitokea Ethiopia na Usomali na baadhi yao walipigwa kihorera na wafanya magendo na kutupwa majini kutafunwa na mapapa.