Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama kuridhia kuanzishwa ofisi ya kuimarisha amani Burundi

Baraza la Usalama kuridhia kuanzishwa ofisi ya kuimarisha amani Burundi

Baraza la Usalama limepitisha, kwa kauli moja, azimio la kuanzisha ofisi maalumu mpya nchini Burundi (Bureau Integre des Nations Unies au Burundi, BINUB)itakayopewa dhamana ya kusaidia kujenga utulivu wa kudumu nchini baada ya Shirika la UM juu ya Ulinzi wa Amani (ONUB) kukamilisha operesheni zake mwisho wa mwaka (31 Disemba 2006).

Ofisi ya BINUB itaiisaidia Serekali ya Burundi katika kudumisha amani na kuboresha shughuli sa utawala wa kidemokrasia, na pia katika kupunguza umilikaji wa silaha haramu na kuwasilisha mageuzi yanayofaa kwenye sekta ya usalama. BINUB kadhalika inatarajiwa kushiriki kwenye taratibu za kuimarisha haki za kiutu na huduma za maendeleo.