Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yalalama, upungufu wa michango unahatarisha maisha ya mamilioni kusini ya Afrika

WFP yalalama, upungufu wa michango unahatarisha maisha ya mamilioni kusini ya Afrika

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limenakiliwa likiripoti ya kuwa limelazimika kupunguza ile posho ya chakula wanayofadhiliwa watu muhitaji milioni 4 katika eneo la kusini ya Afrika, kwa kima kikubwa zaidi, kwa sababu ya uhaba wa michango kutoka wahisani wa kimataifa.