Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa Idara ya Huduma za Dharuru ya Umoja wa Mataifa ziarani Afrika

Mratibu wa Idara ya Huduma za Dharuru ya Umoja wa Mataifa ziarani Afrika

~Mratibu wa idara ya huduma za dharura ya Umoja wa Mataifa Bw. Jan Egeland akiwa ziarani huko Afrika ya kati alianza ziara yake huko Kongo mashariki, kwa kutemebelea kambi za wakimbizi na watu walioathirika sana na mapigano nchini humo.

TY. Naibu katibu mkuu wa umoja wa mataifa anae shughulikia huduma za Dharura Bw.Egeland baada ya kukutana na viongozi wa serekali kuu ya jamhuri yaki demokrasia ya kongo alitembelea miji ya mashariki na mwanzoni mwa wiki hii alikutana kwanza na kundi la wapiganaji wa kundi la Mayi Mayi waliokwisha pokonywa silaha zao hivi karibuni pamoja na mashariki yasiyo ya kiserekali. Wakati wa mikutano yake amezungumzia juu ya kuendelea kwa ghasia na kutoa mwito wa kusitishwa mara moja mateso dhidi ya wananchi na kukomesha ile hali ya kutoadhibiwa watu wanaotenda maovu. Kituo kimoja ambacho Bw. Egeland alitembelea na kusikitishwa sana ni hospitali ya Panzi huko Bukavu ambako aliwatembelea wanawake wahanga wa ubakaji na mateso. Na alisema tabia hiyo inabidi kusitishwa mara moja

CUT1 Egelandhas treat 10….

AaHospitali ya panzi hiyo imetibu karibu wanawake elfu 10 tangu mwaka 1999 kwa wanawake walobakwa. Ni wanawake walotendewa maovu maovu ya kikatili kabisa. Nilizungumza na baadhi ya wanawake hao shujaa na kunielezea matatizo na machungu yao mnamo wiki chache zilizopita hivyo ghasia zinaendelea..

TYBw. Egeland anasema hali ni ya wasi wasi lakini tatizo kubwa anasema kuna ile tabia iliyo katika nchi hiyo ya hakuna anae hukumiwa kwa maovu na uhalifu wanaotenda.

CUT Egeland 2It has to stop

AaNi lazima tabia hiyo isitishwe mara moja hatuwezi kuacha hali hii ya watu kuhisi hawawezi kuchukuliwa hatua na kuadhibiwa. Tumefanya maendeleo katika sehemu nyingi mfano uchaguzi na juhudi za kuleta amani , lakini hatuwezi kuona hali ya kutowaadhibu wahalifu inaendelea na serekali ya nchi hii hasa haijafanya lolote kuhusiana na hali hii.

TYwakati wa mazungumzo yake na rais Joseph Kabila mratibu wa huduma za dharua alizungumzia suala la maendeleo yaliyopatikana na huduma za dharura nchini humo lakini alisisitiza kua walizungumza juu ya masuala hayo ya ukiukaji haki za kiraia.

CUT 3 Egeland

AAwakati wa mazungumzo yangu na rais Kabila nilimwambia ni lazima hali hiyo isitishwe inabidi papatikane maendeleo katika kulinda wananchi na inahitaji serekali kuonesha kua inachukua hatua kuwakamata na kuwafunga wanaohusika na wasihisi wanaweza kuendelea na tabia hiyo. Alikubali kwamba baada ya serekali iliyochaguliwa na wananchi kuchukua madaraka suala hilo litashughulikiwa vilivyo.

TYBw Egeland baada ya kuitembelea Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ataelekea huko kaskazini mwa Uganda kujionea hali huko na kuelekea juba kusini mwa Sudan kwa mazungumzo na viongozi wa serekali ya Sudan ya kusini.