Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Serekali ya Uganda kutoa msamaha kwa waasi wa LRA hali ikiruhusu

Serekali ya Uganda kutoa msamaha kwa waasi wa LRA hali ikiruhusu

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Uganda, Sam Kutesa aliwaarifu wajumbe wa kimataifa katika Baraza Kuu kwamba serekali yake, ikilazimika, ipo tayari kutoa msamaha kwa viongozi wa kundi la Lord\'s Resistance Army (LRA), kundi la waasi ambalo linajulikana kwa ukatili wa kuwatumia wanajeshi watoto wanaolazimishwa kuendeleza vitendo vya karaha dhidi ya utu, na pia kuendeleza unyanyasaji wa kijinisia dhidi ya wanawake wanaowateka nyara katika Uganda ya Kaskazini. jafanya askari mtoto ambalo limetuhumiwa, katika siku za nyuma, kuendeleza vitendo vya kikatli vilivyoharamisha haki za kiutu dhidi ya watoto na wanawake.

Bwana Kutesa alisema uamuzi huo ni mgumu na unahuzunisha. Lakini baada ya wenye madaraka kushauriana kwa muda mrefu waliafikiana kuwasilisha pendekezo lao, ikiwa katika juhudi za kuukomesha mgogoro uliolivaa taifa lake kwa muda wa miaka ishirini. Bw. Kutesa alitahadharisha ya kuwa pendekezo lao la kutoa msamaha halimaanishi katu kwamba Serekali ya Uganda inakubaliana ile tabia ya kuwapatia uhuru wa kutoadhibiwa wale raia wanaofanya makosa ya jinai. Alikumbusha ya kuwa mwezi iliopita licha ya kuwa LRA na Serekali ya Uganda walitiana sahihi maafikiano ya kusitisha uhasama na mapigano kati yao katika maeneo ya kaskazini na mashariki, tusisahau ya kuwa baadhi ya viongozi wa LRA wameshafunguliwa, rasmi, mashitaka dhidi yao na ile Mahakama Kuu ya Kimataifa Dhidi ya Makosa ya Jinai ya Halaikia (ICC). Kadhalika alikumbusha ya kuwa mapatano ya amani ya jumla bado hayajawasilishwa kati ya LRA na Serekali ya Uganda.