Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Amani ya Kimataifa

Umoja wa Mataifa unaadhimisha Siku ya Amani ya Kimataifa

Alkhamisi, tarehe 21 Septemba iliadhimishwa na Umoja wa Mataifa (UM), kote duniani, kuwa ni Siku ya Amani ya Kimataifa. Katibu Mkuu Kofi Annan alijumuika kwenye Makao Mkuu mjini New York na watu mashuhuri kadha walioteuliwa na UM kuwa wajumbe wa kuendeleza mbele kampeni ya kuimarisha amani ulimwenguni, akiwemo pia Daktari Jane Goodall, kwenye tafrija za kuiadhimisha Siku hiyo. Daktari Goodall ni mtafiti wa wanyama pori na mtetezi wa hifadhi za mazingira, na ni mtu maarufu Afrika Mashariki ambapo alifanyia tafiti zake muhimu kadha wa kadha juu ya tabia za wanyama pori hususan masokwe.