Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yawakilisha ripoti kuhusu maamirisho ya lengo la MDGs juu ya maji safi na usafi wa mastakimu

UNICEF yawakilisha ripoti kuhusu maamirisho ya lengo la MDGs juu ya maji safi na usafi wa mastakimu

Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Ann Veneman Alkhamisi aliwakilisha mbele ya waandishi habari wa kimataifa, ripoti yenye kuelezea maendeleo yaliopatikana kuhusu utekelezaji wa lengo la MDGs la kuimarisha huduma za maji safi na usafi wa mastakimu. Kwa mujibu wa ripoti ya UNICEF, tangu 1990 watu bilioni 1.2 walifanikiwa uwezo wa kupata maji ya kunywa safi na salama.

Bi Maria Mutagamba, Waziri wa Maji na Mazingira wa Uganda alijumuika na Veneman kwenye mazungumzo na waandishi habari wa kimataifa kwenye Makao Makuu. Waziri Mutagamba alipongeza juhudi za UNICEF katika kuyasaidia mataifa ya KiAfrika kukabiliana na tatizo la maji safi na usafi wa maskani.

Sikiliza ripoti kamili kwenye idhaa ya mtandao.