Maelfu ya wahamiaji wa Usomali wakimbilia Kenya kunusuru maisha

29 Septemba 2006

Shirika la UM juu ya Miradi ya Chakula Duniani (WFP) limeripoti ya kuwa maelfu ya wahamiaji kutoka Usomali wanakimbilia Kenya hivi sasa kukwepa mapigano yaliofumka karibuni nchini mwao baina ya wafuasi wa Umoja wa Mahakama za Kiislamu (ICU) na vikosi vya Serekali ya Mpito.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Serekali ya Mpito ya Usomali, Ismael Mohamoud Hurreh aliwaambia wajumbe waliohudhuria mjadala wa mwaka wa Baraza Kuu kuwa Serekali yake itasita kushiriki kwenye mazungumzo ya upatanishi ikiwa Umoja wa Mahakama za Kiislamu (ICU) utaselelea kuendeleza kile alichokiita “sera za ugomvi na unyakuzi ziada wa maeneo” nje ya Mogadishu.

Waziri wa Masuala ya Nchi za Kigeni wa Kenya, Raphael Tuju katika mazungumzo na Idhaa ya Redio ya Umoja wa Mataifa alisema tatizo la Usomali linapewa umuhimu na taifa lake kwa sababu machafuko ya Usomali huathiri pia usalama wa Kenya.

Sikiliza taarifa kamili kwenye idhaa ya mtandao.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud