Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa kuisifu Serikali ya JKK

Jumuiya ya kimataifa kuisifu Serikali ya JKK

wiki hii jumuiya ya kimataifa imeisifu serekali ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa kufanikiwa kutayarisha na kufanya uchaguzi wa kwanza kabisa wa vyama vingi katika kipindi cha zaidi ya miaka 40 iliyopita.

AA Uchaguzi huo ulofanyika mwisho wa mwezi wa July ulikua wa kwanza mkubwa kabisa kugharimiwa na kuandaliwa na umoja wa mataifa. Katibu mkuu Koffi Annan katika taarifa yake alitoa mwito kwa vyama vyote vya Kongo na wagombea viti vya uchaguzi huo wa rais na bunge kuheshimu matokeo yake. Lakini, mwandishi habari huru wa mjini Beni, kaskazini mashariki ya Kongo, Molelwa Mseke Dide anasema siku moja tu baada ya kuanza kuhesabiwa kura kulizuka malalamiko.

Dide 1 “Siku moja tu baada ya kutolewa matokeo kulitokea malalamiko …..redio ya OKAPI….kuna wizi na udanganyifu katika uchaguzi huo…. Watu wa Bembe wanaema hawautambui uchaguzi kama uliendeshwa kwa uwazi. ”

AA Akiulizwa na radio ya UM juu ya namna redio hizo zinapata matokeo hayo, msemaji wa tume huru ya uchaguzi huko DRC Bw Diedone Murime Mulongo, anasema :

Mulongo: “Wanapata kutoka vituo vya kura (q2)….wangoje wakati sisi tutajumlisha matokeo court supreme…resulta provisiore. “

AA. Tume ya uchaguzi hivi sasa imewataka wagombea wote wasubiri kura zihesabiwe na kuweza kufikisha malalamiko yao mbele ya mahakama kuu, ili uwamuzi wa dhati uweze kuchukuliwa. Cha kucutia katika uchaguzi huo ambao wachambuzi wengi na watu wengi hawakutarajia utafanyika kwa amani na utulivu, ni kwamba makundi ya waasi ambayo bado hayajaweka silaha zao chini hasa huko mashariki na kaskazini mashariki ya Kongo wamesifu namna uchaguzi ulivyo fanyika. Na mwandishi habari Molelwa Msekwa anasema;

DIDIE 2 Bila shaka wamefurahishwa sana na wengi wamesema kua wao wako tayari ….hakubaliani na matokeo hayo.

AA Afisi ya umoja wa mataifa huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo MONUC ilitoa mwito kwa wagombea wote na vyombo vyote vya habari kustahamili na kusubiri hadi kazi za kuhesabu kura zimemalizika kabla ya kutoa malalamiko. Mwakilishi maalum wa katibu mkuu huko Kongo William Lacy Swing alisema ni kwa maslahi ya wananchi na utaratibu kamili kwa watu kua na subira na utulivu. MONUC imesema tume ya uchaguzi na mamlaka ya vyombo vya habari ya serekali zitafunga kituo chochote cha radio kitakacho toa habari za awali. Na msemaji wa IEC Bw Murime Mulongo anasema changa moto kubwa hivi sasa ni kukusanya pamoja kura kutoka kila pembe ya nchi na kufikisha katika kituo kikuu cha hesabu.

Mulongo “ kazi kubwa tunayo kabisa ….. usalama…waangaliye jinsi kazi itafanyika hapo maana tunapenda kazi ifanyike kwa wazi kabisa.

AA Wakuu wa umoja wa mataifa wamewasifu wananchi wa Kongo kwa kuonesha busara, hikma na adabu kwa kuendesha uchaguzi huo kwa utulivu. Wakongo millioni 25 walikuwa wamejiandikisha kupiga kura kuchagua kati ya wagombea 32 wa kiti cha rais na zaidi ya wagombea elfu 9 wa viti vya Bunge. Katibu Mkuu Koffi Annan amesema UM utaendelea kuisadia nchi hiyo katika juhudi zake za kuimarisha amani ya kudumu na kidemokrasia.

TMY: Na kwa hayo tunahitimisha matangazo yetu kwa wiki hii. Mpaka wiki ijayo kwa taarifa nyengine kuhusu UM, na kwa niaba ya Abdushakur Aboud, ni mimi TMY nikikuombeeni nyote amani, na kwaherini.