Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya UKIMWI - Toronto Canada

Mkutano wa Umoja wa Mataifa juu ya UKIMWI - Toronto Canada

Katika makala ya leo tutazungumzia juu ya mkutano wa 16 juu ya UKIMWI unaomalizika huko Toronto Canada. Kwa wengi wanahisi mkutano ulifanikiwa ingawa hapakua na tangazo lolote la kupatikana tiba au dawa mpya ya kupambana na virusi vya HIV.

RM: Kwa kweli kwa sababu tumekuwa na shida ya huu ugonjwa wa UKIMWI nchini hasa kwa vijana wetu walioko mashuleni na tuna mipango ambayo tunayo ili kuwasaidia hao wanafunzi wetu hapo nchini. Kwa hiyo tuliona ni vyema tukaja kwenye huu mkutano mkubwa wa dunia ili kuona wenzetu kutoka nchi mbali mbali wanafanya nini.

AA:Na kwa hivyo katika siku tuko hapa ni mipango gani ambao mmeona ambayo yanavutia au yanaweza kufanana kua na faida kwenu au mipango gani ambao mnahisi nyinyi … mubadilishe mikakati?

RM:Kwa kweli mipango ambayo tunayo nchini ni nzuri tu lakini hii mipango mengine ambaye tumejifunza kutoka sehemu mbali mbali nchini ninaamini itatusaidia sana kuweza kujimarisha kikamilifu nchini kuhusu ugonjwa wa UKIMWI.

AA:Sasa ni mipango hasa gani ambalo unaweza kutufafanulia kuhusu vijana manake swala kubwa hapa ni kwamba sauti ya vijana imekua haisikiki. Kwa hivyo wanataka sauti ya vijana isikike. Kwa hivyo nyinyi mipango yenu kuhusu vijana ni yepi?

RM:Mipango yetu kuhusu vijana wetu hapa nchini tunawapa masomo kuhusu huu ugonjwa wa UKIMWI, athari zake na wafanye nini ili waipukane na huu ugonjwa wa UKIMWI.

AA:Kwa hivyo unaweza kusema ni mipango ilioko katika shule, katika masomo, ni mada maalum ya masomo au vipi?

RM:Katika mitala yetu tumeihusisha UKIMWI katika baadhi ya masomo uchukuzi, kama somo la historia, somo la civic, somo la biology.

AA:Kwa hivyo katika mkutano kama huu, mipango kama hiyo munapata faida gani hasa. Je kuna mbali ya nchi na nchi au makundi na makundi na mashirika mbali mbali, ni misaada ya aina gani munaweza kupata kuweza kuendeleza mipango hiyo yenu?

RM:Lengo kubwa ni upungufu wa fedha. Ninaamini tukipata fedha zaidi nchini tutaweza kuimarisha hawa vijana na vile vile tukaandaa materials mbali mbali ambazo vijana wetu wanaweza wakazisoma.

AA:Ukiangalia katika hapa mmoja kati ya swala kubwa hata ripoti ya Umoja wa Mataifa juu ya UKIMWI hii leo imesema asilimia hamsini ya vijana ingawa wanajua UKIMWI lakini bado hawafahamu undani na UKIMWI yenyewe. Hasa unaweza kutufafanulia zaidi swala hilo, takwimu hizo ni ya juu kabisa?

RM:Niseme kwamba nchini tumejitahidi kuwaelimisha hawa vijana wetu kushu athari za UKIMWI, wanafunzi wetu wa shule za msingi, wanafunzi wetu wa shule za sekondari, hata wanafunzi wetu wa vyoo vya walimu. Naweza nikasema kwamba kuna mwamko – at least wanafahamu.

AA:Kwa hivyo wakiwa wanafahamu, halafu utakuta kwamba fedha mingi au mipango mingi imekua ikifanyika katika miji. Lakini ukienda vijijini watu bado wako mbali kabisa na swala hilo. Ni jambo gani mnalofanya, hata huko Tanzania, nimezungumza na baadhi ya watu wamesema walifanya utafiti kule katika vijiji ambapo hakuna vyombo vya habari au hakuna njia ya watu kupata habari. Ni namna gani au mipango gani mnafanya kuweza kuwaelimisha zaidi watu wa vijijini kuliko mjini?

RM: Bahati nzuri nchi tuna kanda zetu nane za elimu na katika hizi kanda tuna magazeti ambayo yanatayarishwa. Sasa katika hayo magazeti kuna taarifa ambazo zinaandikwa kuhusu ugonjwa la UKIMWI. Na bahati nzuri redio yetu ya Tanzania kwa sasa inasika nchi nzima. Kwa hiyo hata hao wa vijijini wanapata elimu kuhusu UKIMWI.

AA:Na katika huko Tanzania manake kila nchi ina matatizo yake mbali. Kwa upande wa vijana nini hasa mnasikia ndio changamoto au matatizo yanaokabili vijana kuhusu upande wa UKIMWI manake katika nchi za … wengine wanadharau wanaona hii ni mambo ya ni uongo na kadhalika. Huko Tanzania hali iko namnagani?

RR:Ninaweza nikasema kwa sasa kuna mwamko mzuri kwa kweli hasa katika wanafunzi walioko katika shule zetu za mjini. Ninasema hivi kwa sababu hata maswala ya mimba mijini yamepungua sana sana. Kwa hiyo at least wana ile elimu.

AA:Kwa hivyo hivi sasa mtu akisikia mazungumzo haya atasema unaposikia mkutano wa UKIMWI watu walikua wakifikiri ni swala la afya peke yake, mmekuja pamoja kwa upande wa elimu ..wengine kadhalika. Sasa unaweza kuwaeleza wasikilizaji mkutano kama huu manake ni mkubwa watu elfu 24, mada muhimu nafikiri mnavyojadili, mnaweza kufwatilia yote au vipi mambo yanafanyika katika mkutano kama huu?

RM:Kwa kweli tumefurahi sana kuona kwamba katika mkutano huu mada ni nyingi sana. Lakini tulichofanya ni kuangalia ni mada zipi ambazo tunafikiria zinaweza zikasaidia huko kwetu nchini Tanzania na ambazo tumejaribu kuhudhuria katika hizo mada. Na bahati nzuri kuna maandishi vile vile ambayo yapo, kwa hiyo tunaamini maandishi hayo yatatusaidia vile vile.

AA:Na labda ya mwisho ni kwamba swala kubwa ni kwamba watu wamekua wakizungumza miaka 25 tangu UKIMWI kujulikana, watu wanasema ni wakati wa utekelezaji. Vipi swala hilo hapa katika mkutano unaweza kuwaeleza wasikilizaji unachukuliwa?

RM:Niseme tu kwamba imekua nafasi pekee kwamba tumekua exposed kwa maandishi mbali mbali, tumekua exposed kwa wataalam mbali mbali, vile vile tumepata nafasi ya kuhudhuria hizi lectures mbali mbali – Mimi naamini hizo zote zimetusaidia sana kwamba tumeimarika na tukirudi nchini baasi tutajitahidi kuwambia wenzetu ambao tunafanya nao kazi na wananchi kwa ujumla na wanafunzi.

AA:Na hatimaye, nini hasa kilichokuvuta wewe zaidi ambao unafikiri kimekuwa cha manufaa ambacho unaweza kuondoka nacho hapa?

RM:Kilichonivutia zaidi nikuona kwamba nchi mbali mbali ziko very serious na hili jambo na ndio maana kama nilivyosema pale mwanzoni tunawashiriki 24 elfu ambalo sio kitu kidogo. Kile kitu mimi kimenipa moyo sana.