Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UKIMWI - Mkutano wa Toronto

UKIMWI - Mkutano wa Toronto

Suala la wanawake na watoto ilipewa kipaumbele kwenye mazungumzo ya Toronto, hasa kulitolewa mwito kuwapatia wanawake mamlaka zaidi ili waweze kujikinga kutokana na ghasia na tumiaji nguvu dhidi yao.

JC:Katika kazi zetu hasa kwa upande wa wanawake kwenye global village kuna network zone wanawake wote wanaofanya kazi katika sehemu mbali mbali wanajaribu kuzieleza kazi zao na wanajaribu kuonyesha program zao kwamba zinavyoweza kusaidia kupunguza mambukizi ya virusi vya UKIMWI. Kuna sehemu ya sex workers nao kuonyesha matatizo wanayoyapta wanapokua na clients wao wanapokuwa wanawasisitiza watumia condom na wakakuta kwamba clients hawataki kutumia condom. Vile vile tuna vikundi vingine vya kina mama ambao wana kazi zao za mikono wanaonyesha jinsi wanavyojaribu kuboresha maisha yao kwa kuuza hivyo vifaa vyao vya kazi za mikono. Pia tuna sehemu nyingine ya sheria, inaweza matatizo wanaopata wanawake hasa wanapotaka kupata haki. Na vile vile tumekua tunajifunza pia maana tunakua na workshop mbali mbali pia, jinsi wanawake wanavopata hii women violence, hasa wasichana wa miaka 15 mpaka 24. Kuna wengine pia wanajikuta kwamba wamekua raped kwa.. zile imani za kitamaduni labda mtu akitembea na mwanamke ambae ni virgin anaweza asipata mambukizi ya virusi vya UKIMWI. Lakini sasa tunaona kwamba hiyo amani.. inafanya kwamba watoto wengi katika umri mdogo wanabakwa, kwa hiyo inakua ni vibaya sana kwa sababu wanaanza kupata mambukizi wakiwa katika umri mdogo.

AA: Kwa hivyo swala hilo lilipozungumzia manake limeinia katika nchi nyingi za Afrika, je katika mkutano huu linajadiliwa na njia za suluhisho zinajadiliwa?

JC:Linajadiliwa kwa kina na wengi wameona kwamba katika nchi mbali, kuna nchi zingine ambazo zina sheria ya UKIMWI na kuna nchi zingine hazina. Kwa hivyo wanajaribu kujadili kwamba yaani kwa ujumla wetu kiulimwengu kwamba sheria zilizopo ziweze kufanyiwa marekibisho. Kuna nchi zingine ambazo tayari zimeshaweka sheria kali. Kama Tanzania sasa hivi kama unambaka msichana wa umri mdogo au kijana wa umri mdogo kuna sheria unaweza ukafungwa hata miaka thelathini au pia ukafungwa maisha. Kuna nchi zingine ambazo hazijawa na hizo sheria na nchi zingine zile sheria zilizopo bado haziwezi kukidhi mahitaji. Kwa hiyo majadilano yanaenda kwamba ni jinsi gani wataweza kufanya ili angalau tuwe na sheria ambazo zitaweza kubana na kuzuia hivi vitendo.