Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa Utendaji wa UM Kudhibiti Silaha Ndogo Ndogo Wafanyiwa Mapitio

Mpango wa Utendaji wa UM Kudhibiti Silaha Ndogo Ndogo Wafanyiwa Mapitio

Miaka mitano baada ya Umoja wa Mataifa (UM) kupitisha Mpango wa Utendaji wa kukabiliana na biashara haramu ya silaha ndogo ndogo na silaha nyepesi katika dunia, Makao Makuu ya UM yalishuhudia mkusanyiko wa hali ya juu wa wawakilishi karibu 2,000 wa kimataifa kutoka serikali wanachama mbalimbali, pamoja na mashirika ya kikanda na kimataifa kwa makusudio ya kuzingatia uwezekano wa kulikomesha tatizo la kuenea kwa silaha ndogo ndogo na silaha nyepesi katika ulimwengu.

Dktr Raphael Masunga CHEGENI, mbunge wa kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alikuwa miongoni ya wawakilishi wa kimataifa waliohudhuria kikao hiki cha UM. Alifanya mahojiano maalumu juu ya tatizo la silaha ndogo ndogo na Redio ya UM.

Kwa maelezo kamili sikiliza matangazo.