Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa kimataifa washindwa kuhudumia raia muhitaji katika jimbo la Sudan la Darfur

Wafanyakazi wa kimataifa washindwa kuhudumia raia muhitaji katika jimbo la Sudan la Darfur

Shirika la UM juu ya Operesheni za Amani katika Sudan, UNMIS, limeripoti karibuni ya kuwa wafanyakazi wa kimataifa wanaosimamia huduma za kiutu katika Darfur wanakabiliwa na vizingiti vinavyokwamisha huduma za kuwasaidia raia kupata mahitaji ya kunusuru maisha kwa sababu ya kuendelea kwa mashambulio na hali ya utumiaji nguvu dhidi yao, pamoja na vitendo vya uharamia na mapigano yalioshtadi kati ya makundi ya waasi.~~

Wiki iliopita katika kambi wa wahamiaji wa IDP ya Hissa Hissa, iliopo Darfur ya Magharibi wafanyakazi watatu wa Shirika la Maji la Serekali ya Sudan walizongewa na kupigwa na wahamiaji wa IDP mpaka wakafa. Watumishi hao wa Serekali walikwenda kwenye kambi ya wahamiaji kupima usafi wa maji. Mwakilishi wa KM kwa Sudan, Jan Pronk ameshtumu vikali mauaji haya na kukumbusha ya kuwa Shirika la Maji la Serekali ya Sudan ni mwenzi mkuu wa Shirika la UM juu ya Mfuko wa Maendeleo ya Watoto (UNICEF) na wameshiriki katika huduma kadha za kusaidia kihali ule umma ulioathirika na ugomvi na mapigano katika Darfur. Pronk aliwataka viongozi wa jamii za kambi za wahamiaji wa ndani ya kuchukua hatua zote zitakazohakikisha mashambulio kama haya hayatoibuka tena katika maeneo yao.