“Maisha baada ya vita” ni maonesho mapya ya picha yanayofanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani yakilenga kuchunguza jinsi upendo wetu wa kina na muungano wetu unavyo tuunda wakati wa kipindi cha hatari na kupoteza, na namna unavyotusukuma kuishi hata baada ya vita kuisha.
Baada ya familia ya mume wake kugundua kwamba alifanyiwa ukatili na kubakwa wakati wa vita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, walisisitiza kuwa ingekuwa bora kwa watoto wake kutoishi na mama yao.
Elodie alikuwa na umri wa miaka 17 wakati jiji alilokuwa anaishi lilipo vamiwa na watu wenye silaha.vyeye pamoja na marafiki zake wa kike walishambuliwa na watu wanne wenye silaha na kubakwa.
Wanaume hao walimwagia Elodie kemikali kwenye macho yake na akahisi maumivu makali na kuungua. Uwezo wake wa kuona umekuwa ukiwa ukiendelea kupungua kila mara mpaka akawa kipofu.
Kwa kuwa alijifunza kupika tangu anagali mdogoutotoni, bado anafurahia kupika licha ya kuwa kipofu
Anamsaidia mama yake na dada yake katika biashara yao ndogo ya upishi. Yeye huandaa chakula kila siku kwa ajili ya kwenda kuuzwa baadaye katika soko la jirani.
"Ni muhimu kuwa na njia mbadala; mtu lazima ajifunze jinsi ya kuishi," anasema Charles.
Akiwa amepoteza kila kitu wakati wa vita nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Charles aliamua kurejea shuleni. Baada ya kuhitimu kutoka shule ya upili, alijiunga na Chuo cha Sanaa na masomo ya mawasiliano.
"Baada ya kutoka shule, mimi hufanya kazi kama dereva wa pikipiki mpaka usiku sana. Ninakuwa kwneye hatari nyingi sana wakati nafanya kazi hii kwani Bangui sio jiji salama. Lakini haya ndiyo mambo ninayopaswa kufanya ili kusaidia familia yangu," amesema Charles.
Eneo lote la jirani alilokuwa akiishi Elise lilikuwa limevamiwa. Wanaume wawili waliovalia mavazi ya kijeshi yaliyochakaa walimfanyia ukatili na kumbaka.
Alifanikiwa kukimbilia eneo lenye usalama. Akiwa hospitalini alipatiwa matibabu ya kiwewe pamoja na maeneo mengine ya mwili wake yaliyopata majeraha lakini hakuwaeleza kuhusu kubwaka kwa sababu aliona aibu. "Nilikuwa na mwanamume wakati huo, sikutaka kumjulisha kuwa wanaume wengine walikuwa wameingilia mwili wangu."
Maisha baada ya vita inaangazia kazi za wapiga picha walioshinda tuzo ambao ni Rena Effendi, Pete Muller na Finbarr O'Reilly.
Imeandaliwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC kwa ushirikiano na Mfuko wa wakfu wa waathirika pamoja na Taasisi ya Carmignac.
"Maisha Baada ya vita: Ni simulizi zilizotolewa na ICC kitengo cha kuifikia jamii na waathirika wa uhalifu mbaya ulimwenguni “ maonesho haya yatamalizika tarehe 29 Julai 2022.