
Hend (mwenye umri wa miaka 12): "Tulikuwa kwenye basi, barabara ilikuwa mbaya sana, kulikuwa na shambulio la bomu na tuliweza kusikia milio ya risasi. Maisha yangu yamebadilika. Nawakumbuka rafiki zangu. Hivi sasa kuna takribani wayemen milioni 30 na kati yao hao, milioni 20 wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Hala, (mwenye umri wa miaka 11) "Nina wanasesere wangu wote Hudaydah. Gari na wanasesere. Ninapenda zaidi mwanasesere. Halikadhalika rafiki yangu Maryam. Ninafurahia sana ninapokwenda shuleni na kucheza.
Mama yake Maryam anasema, "tukila kifungua kinywa, hatuli mlo wa mchana. Na iwapo hatutakula milo yote basi tutakula mlo wa usiku."
Umoja wa Mataifa unasema Yemen inakabiliwa na baa la njaa mwaka huu wa 2021.

Kamal (mwenye umri wa miaka 35) "Mwanangu wa kiume ana ugonjwa wa moyo. Matibabu yake hayapatikani hapa; nachukua dawa kutoka Hudaydah. Kitu ninachojivunia mwanangu ni kwamba ananifanya niendelee kuishi."
Zaidi ya asilimia 80 ya wilaya za Yemen zinahitaji msaada mkubwa wa huduma za afya.

Fathi (mwenye umri wa miaka 48): "Nina watoto watano na sasa sina kazi kwa sababu niliumia mgongo. Sijui la kufanya kumudu yote sasa."
Umoja wa Mataifa unasaka dola bilioni 3.85 kwa ajili ya msaada kibinadamu Yemen.
Tazama picha zaidi kuhusu taswira ya Yemen hapa.