Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

30 Oktoba 2020

Katika kuelekea siku ya miji duniani hapo kesho Oktoba 31, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Abtonio Guterres kupitia ujumbe maalum wa siku hiyo amesema miji imebeba gharama kubwa ya janga la corona au COVID-19 lakini jamii katika miji hiyo zimedhihirisha thamani yake katika kukabiliana nalo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP kwa kushirikiana na serikali ya Kenya leo wamezindua mpango wa ugawaji fedha taslim kwa familia 24,000 mjini Mombasa  katika makazi yasiyo rasmi ambao Maisha yao yamesambaratishwa na athari za janga la COVID-19.

Sauti
10'48"