Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Uwekezaji mkubwa kama huu wa bwawa katika Mto Nura nchini Kazakhstan mara nyingi unahitaji uwekezaji wa moja kwa moja wa nje.
World Bank/Shynar Jetpissova

COVID-19 imeangusha kwa asilimia 49 aina zote za uwekezaji wa nje wa nchi zilizoendelea.

Mtiririko wa uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni kimataifa, FDI, umepungua kwa asilimia 49 katika nusu ya kwanza ya 2020 ikilinganishwa na mwaka 2019, kwa sababu ya kuanguka kwa uchumi kutokana na COVID-19, umebaini utafiti wa hivi karibuni wa  Monitor mwelekeo wa uwekezaji uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD na kutolewa leo tarehe 27 Oktoba 2020.