Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UNAMID/Albert González Farran

Utafiti waonesha mtoto 1 kati ya 6 anaishi katika umaskini uliokithiri.

Tathimini ya utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Benki ya Dunia iliyotolewa hii leo mjini New York na Washington DC Marekani imekadiria kuwa mtoto 1 kati ya 6 au sawa na watoto milioni 356 duniani kote, walikuwa wanaishi katika umaskini uliokithiri hata kabla ya janga la virusi vya corona, na hali inategemewa kuwa mbaya zaidi. Ahimidiwe Olotu na maelezo zaidi.

Sauti
3'5"
Covid-19 imesukuma watu kutumbukia katika umasikini zaidi.
© UNICEF/Fazel

Mtoto 1 kati ya 6 anaishi katika umaskini uliokithiri-Utafiti 

Tathimini ya utafiti uliofanywa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na Benki ya Dunia iliyotolewa hii leo mjini New York na Washington DC Marekani imekadiria kuwa mtoto 1 kati ya 6 au sawa na watoto milioni 356 duniani kote, walikuwa wanaishi katika umaskini uliokithiri hata kabla ya janga la virusi vya corona, na hali inategemewa kuwa mbaya zaidi.

Sauti
3'5"