Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© UNICEF Nepal

UNICEF yajiandaa kwa ajili ya chanjo dhidi ya COVID-19

Wakati duniani inasubiri kwa hamu chanjo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICF, nalo limeanza maandalizi ya kuhakikisha chanjo hiyo inatolewa na kusambazwa mapema na kwa usalama kwa kununua na kuhifadhi mabomba ya sindano na vifaa vingine vya kufanikisha zoezi hilo.

Sauti
2'37"
Mhudumu wa afya akijaza bomba na dozi ya chanjo katika kambi ya warohingya ya Cox's Bazar nchini Bangladesh.
© UNICEF Patrick Brown

UNICEF kuandaa sindano na mabomba ya utoaji chanjo dhidi ya COVID-19 