Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Gonjwa la COVID-19 limeumbua ukosefu wa maandalizi-Guterres

Miezi 9 tangu kusikia kwa mara ya kwanza kuhusu ugonjwa wa Corona au COVID-19, janga hilo tayari limeshasababisha vifo vya watu zaidi ya milioni moja miongoni mwa zaidi ya watu milioni 30 waliothibitika kuwa na ugonjwa huo katika nchi 190.

Sauti -
2'12"

07 Oktoba 2020

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo amezindua tamko lake la kisera lenye mapendekezo matano ya kuchagiza mpango wa huduma ya afya kwa wote, UHC kwa lengo la kukabili vilivyo janga la COVID-19 hivi sasa pamoja na kuepusha majanga kama hayo siku za usoni.

Sauti -
11'49"

Wataalamu wa afya TANZBATT 7 wapatiwa mafunzo dhidi ya COVID-19

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC shughuli za ulinzi wa amani zinazofanywa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wa kikosi cha 7, TANZBATT 7 cha kikosi cha kujibu mashambulizi FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani MONUSCO zinaendelea sambamba na kuelimishana jinsi ya kujikinga na gonjwa la Corona au COVID-19 ambalo bado ni tisho duniani.Luteni  Issa Mwakalambo, Afisa Habari wa TANZBATT 7 amefutilia mafunzo hayo na kutuandalia taarifa hii kutoka Beni jimboni Kivu Kaskazini. 

Pikipiki za magurudumu matatu na mashua kutumika kusambaza chakula na pesa Nigeria

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP na serikali ya Nigeria wamezindua programu ya msaada wa chakula na fedha taslimu katika maeneo matatu ya mijini yaani Abuja, Kano na Lagos ambako kote huko ni kitovu cha COVID-19 nchini humo.