Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

06 Oktoba 2020

Harakati za Umoja wa Mataifa za kutekeleza lengo namba 5 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs la usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake linaendelea kupigiwa chepuo na wadau mbalimbali likiwemo shirika la kiraia la Naserian wilayani Monduli mkoani Arusha nchini Tanzania.

Vita vinavyoendelea Mashariki mwa Ukraine vimeongeza madhila kwa maelfu ya wazee na sasa janga la corona au COVID-19 imekuwa ni kama msumari wa moto juu ya kidonda.

Kambale wageuka kichocheo cha uchumi kwa wanawake wa Ibadan Nigeria

Audio Duration
13'7"