Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

05 Oktoba 2020

COVID-19 yamlazimisha mwalimu kusaka kipato mbadala nchini Uganda. UN-HABITAT yachukua hatua kupambana na COVID-19 hata kwa wasio na makazi Kenya. Elimu ya IFAD yawasaidia wanawake wa Kontagora, Nigeria kuwa mamilionea.  

Sauti
13'19"
Mradi wa UN-HABITAT nchini Kenya unaosaidia wasio na makazi katika kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona.
UN News/ Jason Nyakundi

UN-HABITAT yachukua hatua kupambana na COVID-19 hata kwa wasio na makazi Kenya

Ikiwa leo ni siku ya makazi duniani, kuwa na makazi bora imeelezwa hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote ni suala la uhai na kifo hasa janga la corona  au COVID-19 likiendelea kusambaa duniani na watu wakitakiwa kusalia majumbani, lakini hatua hiyo haiwezekani hasa kwa wale ambao hawana wanapopaita nyumbani limesema shirika la Umoja wa Mataifa la makazi UN-HABITAT.

Sauti
2'37"