Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

1 Oktoba 2020

Hii leo mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA75 unakuwa na kikao cha ngazi ya juu kuhusu kuchagiza utekelezaji wa usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake na mtoto wa kike, sambamba na maadhimisho ya miaka 25 tangu mkutano wa 4 wa kimataifa kuhusu wanawake uliofanyika Beijing nchini

Sauti -
13'32"

Watu wenye ulemavu, COVID-19 imetuathiri maradufu-UGANDA

Mwandishi wetu wa Uganda, John Kibego ameangazia changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu hasa wanawake kutokana na vizuizi vilivyosababishwa na mlipuko wa COVID-19 nchini Uganda.

Sauti -
3'24"

Wazee lazima wawe kipaumbele katika juhudi zetu za kuishinda COVID-19-Guterres  

Ulimwengu unaadhimisha miaka 30 ya Siku ya Wazee duniani tunapotathimi athari mbaya na kali ambazo janga la COVID-19 limesababisha kwa wazee ulimwenguni kote, sio tu kwa afya zao, bali pia juu ya haki zao na ustawi wao, amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake alioutoa hii leo kuhusu Siku ya leo ya Kimataifa ya wazee duniani na kisha akashauri.