Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Heko serikali zilizochukua hatua za kijasiri na kuwezesha watoto kurejea shuleni - UNICEF
Ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 ulipovuruga mwenendo wa elimu duniani, kila mtu alisalia na maswali mengi! Je tufanye vipi watoto waweze kuendelea kujifunza? Tufanye vipi ili kuhakikisha watoto wanapata msaada muhimu kupitia shule ikiwemo mlo wenye lishe?
15 Septemba 2020
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema demokrasia ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa taarifa, ushiriki katika ufanyaji maamuzi na uwajibikaji wa kuchukua hatua hasa wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga la corona au COVID-19. Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa mwongozo wenye mapendekezo ya mikakati ya kiafya ya kuzingatiwa na serikali kuhusu linin a jinsi ya kufungua tena shule kwenye maeneo ambako shule bado zimefungwa kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.Hatimaye mamia ya wasaka hifadhi kwenye
Dunia ina fursa kupitia mshikamano wa kimataifa kujijenga vyema upya:Guterres
Katika mkesha wa kuanza kwa kikao cha 75 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA75, Katibu Mkuu António Guterres ameainisha changamoto zinazoikabili dunia na suluhu zinazoweza kupatikana kutokana na ushirikiano wa kimataifa.
Demokrasia ni chachu ya kila kitu katika jamii:Guterres
Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya demokrasia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema demokrasia ni muhimu katika kuhakikisha upatikanaji wa taarifa, ushiriki katika ufanyaji maamuzi na uwajibikaji wa kuchukua hatua hasa wakati huu ambapo dunia inakabiliana na janga la corona au COVID-19.
Wengine bado wakihaha kusubiri kufungua shule, UN yatoa mwongozo wa hatua za kufuata
Mashirika ya Umoja wa Mataifa yametoa mwongozo wenye mapendekezo ya mikakati ya kiafya ya kuzingatiwa na serikali kuhusu linin a jinsi ya kufungua tena shule kwenye maeneo ambako shule bado zimefungwa kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19.