Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Watoto wakimbizi wahusishwa katika kupambana na COVID-19 Uganda
Mlipuko wa COVID-19 duniani umetia mashakani karibu malengo yote ya Maendeleo endelevu au SDGs baada ya kukwamisha elimu, usafiri na uchumi miongoni mwa mengine. Hali imekuwa mbaya zaidi miongoni mwa wakimbizi kutokana na changamoto za uhaba wa rasilimali ambazo kawaida huwakumba hasa idadi yao inapoongezeka bila kutarajiwa. Hata hivyo, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake nchini Uganda wameanzisha ushirikishwaji wa watoto wakimbizi katika juhudi za kupambana na COVID-19 wakati huu ambapo takribani wakimbizi mia moja wameambukizwa. Je, wanashirikishwa vip
Ufadhili, umoja na kuaminiana ni mambo ya lazima kwa ajili ya chanjo ya COVID-19: UN
Viongozi mbalimbali wa Dunia leo Alhamisi wametetea chombo cha kusongesha fursa za nyenzo za kupambana na janga la corona au COVID-19 (ACT Accelerator) wakati huu janga hilo likiendelea kutatiza kote duniani.
Sasa wachambua taka Afrika kusini wafanya kazi kwa kujiamini, kulikoni?
Nchini Afrika Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO na serikali ya Japani limefanikisha usaidizi wa mavazi ya kujikinga mwili kwa waokota na wachambuzi taka ngumu nchini humo ili kuwaepusha na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 .
Mtandao wa maabara mahsusi za kunyumbua virusi vya Corona yazinduliwa Afrika
Wakati nchi za Afrika zikiendelea kupanua huduma za upimaji wa virusi vinavyosababisha Corona au COVID-19, shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na kituo cha Afrika cha udhibiti na kinga ya magonjwa, Africa CDC, wamezindua mtandao wa maabara ili kuimarisha hatua za kuchambua na kufuatilia mnyumbuliko wa virusi vya Corona aina ya 2 kinachosababisha shida kwenye mfumo wa hewa, SARS-CoV-2.