Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Uganda, UNHCR yaimarisha juhudi za kudhibiti COVID-19 miongoni mwa wakimbizi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake nchini Uganda wameimarisha juhudi za kudhibiti vifo na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 miongoni mwa wakimbizi wakati huu ambapo wakimbizi 89 tayari wameambukizwa ugonjwa huo, huku wawili wakiripotiwa ku

Sauti -
2'29"

UNHCR yaimarisha juhudi za kudhibiti COVID-19 miongoni mwa wakimbizi, Uganda 

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na wadau wake nchini Uganda wameimarisha juhudi za kudhibiti vifo na maambukizi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 miongoni mwa wakimbizi wakati huu ambapo wakimbizi 89 tayari wameambukizwa ugonjwa huo, huku wawili wakiripotiwa kufariki dunia.