Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

2 SEPTEMBA 2020

COVID-19 kuwatumbukiza wanawake wengine milioni 47 katika ufukara:UN Women/UNDP.  Familia zinazokimbia mashambulizi Msumbiji zajikuta katika maeneo yaliyoghubikwa na COVID-19.  IFAD imetuwezesha kujenga nyumba na kulala kwenye vitanda- Mkulima Ethiopia. 

Sauti
13'37"
Wakimbizi wa ndani katika maeneo ya Alto Gingone, Pemba mkoa wa Cabo Delgado, Msumbiji
UN Mozambique/Helvisney Cardoso

Familia zinazokimbia mashambulizi Msumbiji zajikuta katika maeneo yaliyoghubikwa na COVID-19 

Mashambulizi katika miji na vijiji vya mkoa wa kaskazini mwa Msumbiji wa Cabo Delgado yamezidi na  kuwalazimisha maelfu ya watu kukimbia kwa miguu, boti au barabara kwenda katika makao makuu ya mkoa ambako ni kitovu cha COVID-19 na ambako shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu ICRC limesaidia kujenga kituo kikubwa cha matibabu kinachofunguliwa rasmi leo, imeeleza taarifa iliyotolewa hii leo na ICRC mjini Maputo. 

Sauti
2'31"