Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.
Taarifa kuhusu Virusi vya Corona
Hata kama corona imetuingilia, bado tunaamini bado maisha yako mbele-Wanafunzi wakimbizi Uganda
Makala ifuatayo inamulika changamoto wanazokumbana nazo wanafunzi wakimbizi ambao hivi sasa wanalazimika kusalia majumbani ndani ya kambi baada ya shule kufungwa nchini Uganda ili kukabiliana na COVID-19. Mwandishi wetu John Kibego anazungumuza na wanafunzi Feza Kabera na Shamil Bao Yahaya ambao wanaeleza jinsi gani wanavyohimili vishawishi vya kupata mimba za utotoni na kujiunga na vikundi vya watumiaji madawa ya kulevya miongoni mwa mengine wakati huu wakiwa majumbani katika kambi ya wakimbizi ya Kyangwali.
Tuitumie COVID-19 kubadili miji yetu:Guterres
atibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kupitia ujumbe wake wa uzinduzi wa tamko la kisera kuhusu janga la virusi vya corona katika miji, hii leo ametoa wito kwa viongozi kote duniani kufikiria upya na kurekebisha miji katika kipindi hiki ambacho dunia inapona kutokana na janga la COVID-19 kwani miji imeonekana kuwa kitovu cha janga hilo. Loise Wairimu na taarifa zaidi
(Taarifa ya Loise Wairimu)
Bwana Guterres ameeleza kuwa miji ni kitovu cha COVID-19 kwa kuwa asilimia ya wagonjwa wote wa janga hili wamethibitika kuwa wa mijini.
Janga la COVID-19 linatupa fursa ya kuibadilisha miji yetu-Guterres
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kupitia ujumbe wake wa uzinduzi wa tamko la kisera kuhusu janga la virusi vya corona katika miji, hii leo ametoa wito kwa viongozi kote duniani kufikiria upya na kurekebisha miji katika kipindi hiki ambacho dunia inapona kutokana na janga la COVID-19 kwani miji imeonekana kuwa kitovu cha janga hilo.