Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Vifo vinavyotokana na VVU, TB na Malaria vinaweza kuongezeka maradufu katika miezi 12 ijayo-Ripoti

Ripoti mpya ya  fuko la kimataifa la ufadhili Global Fund iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi inakadiria kuwa nchi ambazo zimeathirika na Virusi Vya UKIMWI, VVU, Kifua Kikuu yaani TB na Malaria, kwa haraka zinahitaji dola bilioni 28.5 za kimarekani ili kulinda hatua kubwa zilizokwisha kufikiwa katika miongo miwili iliyopita katika mapambano dhidi ya magonjwa hayo matatu.

Wakati wa COVID-19,  sanaa ya kuchora yawa kimbilio la mkimbizi

Kipaji na mapenzi ya uchoraji wa sanaa vimempatia mkimbizi kutoka Eritrea anayeishi nchini Libya faraja na matumaini wakati huu wa zama za janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, linalogubikwa pia na mapigano na kudorora kwa hali ya kiuchum

Sauti -
2'26"

Sanaa ya kuchora yawa kimbilio la mkimbizi wakati wa COVID-19

Kipaji na mapenzi ya uchoraji wa sanaa vimempatia mkimbizi kutoka Eritrea anayeishi nchini Libya faraja na matumaini wakati huu wa zama za janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19, linalogubikwa pia na mapigano na kudorora kwa hali ya kiuchumi na kijamii katika taifa hilo la Afrika Kaskazini.

Tumejizatiti kuepusha maambukizi ya COVID-19 - CCBRT

Nchini Tanzania hospitali ya CCBRT imechukua hatua za uhakika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu, wakiwemo wafanyakazi wake wanajikinga ipasavyo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19.