Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UNICEF VIDEO

Ulemavu alio nao mtoto huyu haukumzuia kusaka kipato kwa ajili ya familia yake

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, athari za janga la virusi vya Corona au COVID-19 zimekuwa mbayá zaidi kwa watoto wenye ulemavu, ambapo mtoto mmoja mkazi wa mji mkuu Kinshasa, ambaye ni kiziwi, amelazimika kusaka mbinu za kuweza kupata kipato ili kusaidia familia yake. John Kibego na maelezo zaidi.

Kinshasa, mji mkuu wa DR Congo katika video hii ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF yenye lengo la kuangazia sauti za vijana katikati ya janga la COVID-19, anaonekana Steve Okito, mtoto mwenye umri wa miaka 14.

Sauti
1'58"
Shughuli za ununuzi kwenye duka jijini Dar es Salaam, Tanzania wakati huu ambapo kumeripotiwa kutangazwa kwa visa vya corona nchini humo.
UN News/ Stella Vuzo

Tanzania inavyokabili janga la corona

Ni miezi miwili na zaidi sasa tangu Tanzania itangaze mgonjwa wake wa kwanza wa virusi vya COVID-19.  Tangu tarehe 16 mwezi wa tatu mwaka huu mengi yamejiri nchini Tanzania kufuatia kuzuka kwa janga la ugonjwa huo unaoathiri dunia nzima.

26 MEI 2020

Katika Jarida maalum la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Walinda amani wawili wanawake mmoja kutoka Brazili na mwingine kutoka India wameshinda tuzo ya Umoja wa Mataifa ya mwanajeshi mchagizaji wa masuala ya kijinsia kwa mwaka 2019. Wanajeshi hao Meja Suman Gawani kutoka India na kamanda Carla Monteiro Araujo kutoka Brazili watakabidhiwa tuzo hiyo Ijumaa ya 29 Meisiku ya walinda amani duniani.

Sauti
9'57"