Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Mbinu dhidi ya virusi vya Corona zachangia uhifadhi wa mazingira- UNEP

Naam na sasa tuelekee nchini Tanzania kusikiliza sehemu ya mchango au ushiriki wa shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP katika mapambano dhidi ya virusi vya corona, COVID-19.

Sauti -
5'39"

25 05 2020

Katika Jarida maalum la habari hii leo Flora Nducha anakuletea

Leo ikiwa ni siku ya Afrika Umoja wa Mataifa umelisihi bara hilo na nchi zinazofanya uchaguzi kudumisha demokrasia wakiendesha uchaguzi huo hata wakati huu wa janga la virusi vya corona au COVID-19

 

Sauti -
9'57"

Afrika fanyeni chaguzi hata katika COVID-19

Umoja wa Mataifa umesihi nchi za Afrika ambazo zinatarajiwa kuwa na chaguzi zama hizi za janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, zitekeleze hatua hiyo ya kidemokrasia ili kusongesha demokrasia na utulivu.