Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

14 Mei 2020

Mwakilishi wa WHO Burundi afurushwa, ofisi ya WHO kanda ya Afrika yazungumza. Huko Sudan Kusini UNMISS yaingia sokoni, kulikoni? Katibu Mkuu wa UN azindua sera ya kusaida afya ya akili wakati huu wa janga la Corona au COVID-19, na mashinani tunakwenda Ituri nchini DRC, kilio cha mama mkimbizi wa ndani na makala ni nchini Kenya. Karibu!

Sauti
12'36"
Dkt. Walter Kazadi Mulombo, Mwakilishi wa WHO nchini Burundi, ( wa pili kushoto) wakati wa uzinduzi wa wiki ya afya ya mama na mtoto mwaka 2019 nchini humo.
WHO/Burundi

Burundi yamfurusha Mkuu wa WHO siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, WHO yazungumza

Shirika la afya la Umoja la Umoja wa Mataifa, WHO, limesema linawasiliana na serikali ya Burundi ili kufahamu sababu ya kufukuzwa kwa mwakilishi wake nchini humo pamoja na wafanyakazi wengine watatu. Serikali ya Burundi ilitangaza jana kumfukuza mwakilishi huyo Dkt. Walter Kazadi Mulombo, ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo. 

Sauti
1'52"