Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Umoja wa Mataifa Bangladesh unatoa kipaumbele kwa huduma zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ambazo zimeathirika zaidi na COVID-19
UNDP Bangladesh/Fahad Kaizer

‘Uharaka wa kuchukua hatua’ kwa ajili ya maendeleo endelevu, ni mkubwa zaidi kuliko wakati mwingine wowote wakati janga la corona likiendelea

COVID-19 ikiendelea inaendelea kuvuruga maisha na ustawi kote duniani, hii leo Jumatatu Umoja wa Mataifa umefanya mjadala mpana wa kisera kusisitiza suluhisho la ushirikiano wa kimataifa ili kupunguza janga wakati pia ulimwengu ukirejea katika mkondo wa kufikia Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu, SDGs.