Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

© UNICEF/UNI322644/Haro

Machifu watumiwa Niger kuhamasisha dhidi ya COVID-19

Kwenye kitongoji cha Banizoumbou katika mji mkuu wa Niger, Niamey, Chifu Yaye Modi Alzouma, anahamasisha wananchi juu ya virusi vya Corona, akisema kuwa hata machifu wamekiri kuwepo kwa gonjwa hilo.

Hatua hii ya Chifu Alzouma ni sehemu ya kampeni zinazoendeshwa kwa ushirikiano na UNICEF zikijumuisha viongozi wa jadi na wapiga debe mjini Niamey.

Kampeni inalenga kuhamasisha jamii ielewa COVID-19, na izingatie kanuni za kutochangamana, na kuheshimu amri ya dharura ya kutotembea hovyo.

Sauti
1'57"

07 MEI 2020

Katika Jarifda la Habari hii leo kwenye Umoja wa Mataifa Flora Nducha anakuletea

-Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF lasema takribani watoto milioni 116 watazaliwa wiki 40 baada ya kutangazwa rasmi kuwa janga la corona limekuwa janga la kimataifa mnano mwezi Machi makwa huu

- Ripoti mpya iliyotolewa leo na ofisi ya Umoja wa Mataifa ya madawa na uhalifu UNODC imesema janga la COVID-19 limeingilia utaratibu wa kusafirisha mihadarati kwa njia ya anga na kuwafanya wafanyabiashara wa bidhaa hizo haramu kusaka njia mbadala

Sauti
12'