Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Guterres:Tukihakikisha haki za wenye ulemavu, tunawekeza katika mustakbali wa Pamoja

Katika mazingira ya kawaida watu wenye ulemavu mara nyingi hukosa fursa ya huduma za msingi kama vile elimu, huduma za afya na fursa za kiuchumi au ushiriki katika jamii.

Sauti -
1'25"

06 Mei 2020

Leo katika Jarida la Umoja wa Mataifa  tunaangazia habari tofauti kutoka sehemu mbalimbali duniani:

-Tutasikia kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu uzinduzi wa sere za  watu wenye ulemavu na janga la corona au COVID-19.

Sauti -
11'18"

UNICEF Kenya yaungana na wafanyakazi wa kujitolea kutokomeza Corona

Nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linashirikiana na jamii ili kusaidia kuepusha kusambaa kwa ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19 hususan kwenye maeneo ya makazi duni

Tukihakikisha haki za wenye ulemavu, tunawekeza katika mustakbali wa Pamoja:Guterres

Katika mazingira ya kawaida watu wenye ulemavu mara nyingi hukosa fursa ya huduma za msingi kama vile elimu, huduma za afya na fursa za kiuchumi au ushiriki katika jamii.