Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Uhuru wa vyombo vya Habari ni chachu ya kukabili COVID-19 na taarifa potofu:UN

Waandishi wa Habari ni kitovu cha kukabiliana na mlipuko hatari wa taarifa potofu zinazoambatana na janga la virusi vya corona au COVID-19 amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Msataifa leo katika mazungumzo kwa njia ya mtandao ya kuchagiza uhuru wa vyombo vya Habari wakati huu wa mgogoro wa kimataifa.

Chama cha wakunga Tanzania tunawashauri wakunga wote kutumia vifaa vilivyotakaswa wakati huu wa COVID-19:Lucy Mabada

 Dunia ikielekea kuadhimisha siku ya wakunga hapo kesho tarehe 5 Mei, Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) kimewapa ushauri wakunga wote kuzingatia kuvaa vifaa muhimu vilivyotakaswa hususani wakati huu wa COVID-19 ili kuwalinda watoto dhidi ya maambukizi.

Sauti -
3'30"

Hakuna aliye salama hadi kila mtu atakapokuwa salama dhidi ya COVID-19:UN

Juhudi kubwa na za kihistoria zinahitajika ili kuweza kulidhibiti janga la mlipuko wa corona au COVID-19 amesema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo alikuhutubia mkutano wa Muungano wa Ulya wa kutoa ahadi ya kupambana na janga hilo uliofanyika kwa njia ya mtandao mjini Brussels.

Mamilioni ya watoto hawataweza kusomea nyumbani-UNICEF

Taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, iliyotolewa leo mjini Nairobi Kenya na Johannesburg Afrika Kusini, imeeleza kuwa zaidi ya watoto milioni 127 wa shule za awali, shule za msingi na sekondari Afrika Mashariki na Kusini, ambao walitakiwa kurejea shuleni wiki hii, wanasalia nyumbani kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19.