Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

UN Photo/Martine Perret

Ni vigumu kwa wananchi kuamini kuwa Ebola imeibuka tena DRC:WHO

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako wagonjwa wapya  wanne wa Ebola wamebainika tangu tarehe 10 mwezi huu wa Aprili, watoa huduma wanaelezea kile ambacho wanakabiliana nacho katika kupambana na mlipuko huu wakati huu ambapo taifa hilo la Maziwa Makuu pia linakabiliwa na ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 na machafuko katika baadhi ya majimbo.

Sauti
1'50"

16 APRILI 2020

Miongoni wa habari ambazo Flora Nducha anakuletea katika Jarida la Umoja wa Mataifa hii leo

- Ubaguzi wa rangi, chuki dhidi ya wageni na hali ya kutovumiliana vimeongezeka wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 kwa mujibu wa mtaalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Tendayi Achiume

-Huko Congo DRC visa vipya vya Ebola vimeripotiwa huku taifa hilo la maziwa makuu likiendelea kukabiliana na majanga mengine kama COVID-19,utapiamlo na vita limesema shirika la afya duniani WHO.

Sauti
12'32"
Wafanyakazi wa kituo cha Ebola cha Katwa Butembo, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC wakisafisha viatu na nguo
UN Photo/Martine Perret

Wananchi DRC hawaamini kuwa Ebola imeibuka tena- WHO

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako wagonjwa wapya  wanne wa Ebola wamebainika tangu tarehe 10 mwezi huu wa Aprili, watoa huduma wanaelezea kile ambacho wanakabiliana nacho katika kupambana na mlipuko huu wakati huu ambapo taifa hilo la Maziwa Makuu pia linakabiliwa na ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 na machafuko katika baadhi ya majimbo

Sauti
1'50"