Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Maji ni muhimu ili makazi duni Kenya yadhibiti COVID-19

Lengo namba 6 la malengo ya maendeleo endelevu, SDG, linalenga kufanikisha upatikanaji wa maji kwa wote na kwa usawa ifikapo mwaka 2030. Lakini bado ulimwenguni kote, kama ripoti ya maendeleo ya maji ya Umoja wa Mataifa, ilivyoonesha, mabilioni ya watu bado wanakosa maji safi na salama na huduma za kujisafi na watu wanaachwa nyuma kwa sababu mbalimbali ikiwemo  ubaguzi kwa misingi ya jinsia, kabila, tamaduni na hali ya kijamii.
 

WHO ina dhima muhimu sana katika kutokomeza COVID-19- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema shirika la afya la umoja huo, WHO linapaswa kuungwa mkono duniani kote, akisema kuwa chombo hicho kimekuwa muhimu sana kikichukua msimamo wa kimataifa kukabiliana na mlipuko wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19.

COVID-19 ina athari kubwa katika saa za kufanyakazi na mapato duniani:ILO

Mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 umeelezwa kuwa na athari mbaya katika saa za kufanya kazi na mapato kote duniani kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika la kazi duniani ILO ambaye inaainisha kanda na sekta zilizoathirika zaidi na kupendekeza sera za kukabiliana na mgogoro huu wa kimataifa.

Unafahamu nini kuhusu vyakula bora hususani wakati huu wa COVID-19?

Mwongozo uliotolewa na Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa FAO unasema japo lishe hutofautiana sana kutokana na mahali na kulingana na upatikanaji wa chakula, tabia za kula na tamaduni, lakini linapokuja suala la chakula, kuna mengi ambayo tunajua juu ya nini na nini sio nzuri kwetu na hii ni kweli bila kujali tunaishi wapi.

Uzoefu tulioupata kukabiliana na ebola unatosha kukabiliana na COVID-19-muuguzi DRC

Wakati mlipuko wa ugonjwa Ebola ukielekea kufikia ukingoni nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, wahudumu wa afya waliopata mafunzo wakati wa janga hilo, hivi sasa wanatumia ujuzi walioupata, kuimarisha mfumo wa afya nchini humo ikiwa  ni pamoja na kutumia uwezo huo kupambana na virusi vy

Sauti -
2'36"

Bara la Afrika japo halina wagonjwa wengi linahitaji msaada ili kudhibiti kusambaa kwa COVID-19-Dkt. Moeti

Wakati janga la mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 likiendelea kuitikisa dunia na kusababisha athari kubwa ikiwemo kupoteza maisha ya maelfu ya watu bara la Afrika mabalo japo halina wagonjwa wengi linahitaji msaada ili kudhibiti kusambaa kwa virusi hiyo.

Sauti -
2'16"

8 Aprili 2020

Assumpta Massoi : Hujambo na Karibu kusikiliza Jarida kutoka Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, kutoka hapa New York Marekani.

JINGLE (04”)

ASSUMPTA:Ni Jumatano 08 Aprili mwaka 2020, mwenyeji wako studioni hii leo ni mimi ASSUMPTA MASSOI

Sauti -
12'13"

Msaada wa kimataifa wahitajika kuepusha mamilioni ya Wazimbabwe na janga la njaa:WFP

Zimbabwe ambayo tayari ina matatizo makubwa ya chakula kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na mdororo wa uchumi sasa janga la mlipuko wa virusi vya Corona unatishia kutumbukiza mamilioni ya watu wa nchi hiyo katika janga la njaa, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP.

Afrika imejiandaa kukabiliana na COVID-19 lakini yahitaji msaada:Dkt. Moet

Wakati janga la mlipuko wa virusi vya Corona au COVID-19 likiendelea kuitikisa dunia na kusababisha athari kubwa ikiwemo kupoteza maisha ya maelfu ya watu, bara la Afrika ambalo japo halina wagonjwa wengi linahitaji msaada ili kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo.

Ujuzi tulioupata wakati wa Ebola tutautumia kupambana na COVID-19-Wauguzi DRC

Wakati mlipuko wa ugonjwa Ebola ukielekea kufikia ukingoni nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, wahudumu wa afya waliopata mafunzo wakati wa janga hilo, hivi sasa wanatumia ujuzi walioupata, kuimarisha mfumo wa afya nchini humo ikiwa na kutumia uwezo huo kupambana na virusi vya corona, COVID-19.