Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Hatua zaidi zachukuliwa kukabiliana na COVID-19 nchini Kenya

Kufuatia raia wa Kenya kulalamikia hatua ya Rais wa nchi hiyo kutangaza zuio la kusafiri katika baadhi ya mikoa kwa mfano kuingia jijini Nairobi, Msemaji wa serikali ya Kenya Cyrus Oguna ameieleza idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa kuwa tangazo hilo la rais Uhuru Kenyatta halina nia ya kumuum

Sauti -
5'26"

UN na wadau Somalia watoa kipaumbele cha kukabiliana na COVID-19

Umoja wa Mataifa na washirika wake wa masuala ya kibinafdamu nchini Somalia wanaweka mipango na vipaumbele vipya ili kusaidia taifa hilo la Pembe ya Afrika katika maandalizi na hatua za kupambana na virusi vya Corona COVID-19.

Fikra za kikoloni katika kujaribu chanjo ya COVID-19 Afrika zikome- WHO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema ameshtushwa sana na kauli za wiki iliyopita kutoka kwa baadhi ya wanasayansi wakipendekeza kuwa majaribio ya kwanza ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona, COVID-19 yatafanyikia Afrika.

Asanteni wauguzi na wakunga na tuna deni kwenu – Guterres

Leo ni siku ya afya duniani ambapo ujumbe ukiwa ni saidia wauguzi na wakunga.

Tunahitaji kuwekeza haraka kuziba pengo la wauguzi duniani:WHO

Mlipuko wa virusi vya Corona COVID-19 unadhidhirisa haja ya kuimarisha jopo la wahudumu wa afya kote duniani , kwa mujibu wa ripoti mpya ya “hali ya wauguzi duniani 2020.”